Tetesi

Liverpool ilijaribu kumwondoa Nunez

LIVERPOOL ilishindwa katika jaribio lake la kumpeleka Darwin Nunez katika timu ya Atletico Madrid kubadilishana na Joao Felix majira haya kiangazi. Joao pia alikataa uhamisho kwenda Manchester United na Aston Villa kabla ya kwenda Barcelona kwa mkopo. (Mundo Deportivo)

Manchester City imekuwa ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya mshambuliaji wa Brighton & Hove Albion, Evan Ferguson na inaamini kwamba ataweza kucheza pamoja na fowadi nyota wa sasa, Erling Haaland.(i news)

Manchester United bado ina nia ya kumnunua kiungo wa Fulham Joao Palhinha, ambaye usajili wake Bayern Munich ulishindikana siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho baada ya klabu hiyo ya London Magharibi kukataa kuidhinisha kuondoka kwake.(The Athletic)

Golikipa Kepa Arrizabalaga amekiri alitaka mabadiliko majira haya ya kiangazi licha ya kocha mpya wa Chelsea, Mauricio Pochettino kumhakikishia nafasi kwenye klabu. Golikipa huyo amefichua kwamba alikataa uhamisho kwenda Bayern Munich ili ajiunge na Real Madrid kwa mkopo.(MARCA)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button