Muziki

Ariana Grande arejea jukwaani baada ya miaka saba

CALIFORNIA: MWIMBAJI, mtunzi wa nyimbo na mwigizaji wa Marekani, Ariana Grande, amerejea rasmi kwenye ziara za muziki baada ya kukaa mbali na jukwaa kwa takribani miaka saba.

Ziara yake mpya ya ‘Eternal Sunshine Tour’ kwa tamasha hilo imefanyika katika ukumbi wa Oakland Arena, California nchini Marekani.

Tamasha hilo lilivutia maelfu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia kurejea kwa staa huyo aliyeshinda tuzo za Grammy. Grande aliwasilisha nyimbo kutoka katika albamu yake mpya ya mwaka 2024, Eternal Sunshine, pamoja na nyimbo zake maarufu zilizomjengea umaarufu duniani.

Ziara hiyo inatarajiwa kuwa miongoni mwa ziara kubwa za muziki mwaka huu, ikihusisha maonesho 41 yatakayofanyika Marekani, Canada na Uingereza. Ziara hiyo ilianza mapema mwezi Juni na inatarajiwa kuhitimishwa Septemba 1 katika ukumbi wa O2 Arena jijini London.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za burudani, Eternal Sunshine Tour ni ziara ya tano ya Ariana Grande na inakuja baada ya kipindi kirefu ambacho msanii huyo alijikita zaidi katika muziki, filamu na televisheni.

Grande amesema ziara hiyo ni hatua muhimu kwake na huenda ikawa miongoni mwa ziara zake za mwisho kwa muda usiojulikana, jambo lililoongeza hamasa kwa mashabiki wake duniani kote.

Related Articles

Back to top button