Habari Mpya

Allison Becker : wachezaji hatusikilizwi

MILAN:Mlinda mlango wa majogoo wa jiji la London Liverpool FC Allison Becker Amesema wachezaji hawana sauti juu ya kuongezwa kwa michezo zaidi kunakofanywa na shirikisho la soka duniani FIFA, shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na mashirikisho ya ligi za ndani.

Becker amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya AC Milan wakati mwandishi mmoja wa habari alipouliza maoni ya golikipa huyo juu ya mfumo mpya wa ligi ya mabingwa barani Ulaya inayorejea tena leo.

“wakati mwingine hakuna mtu anauliza wachezaji kuhusu kuongeza mechi zaidi, pengine labda maoni yetu si kitu, nadhani kila mtu anajua tunavyojiskia kuhusu mechi zaidi. Kila mtu amechoka nadhani sasa ni wakati wa wenzetu kukaa chini na sisi. Tunaelewa watu wanataka mechi zaidi lakini tunahitaji kufanya kitu kuuokoa mpira wa miguu” amesema Allison Becker.

Ikumbukwe michuano inayosimamiwa shirikisho la UEFA msimu huu wa 2024/25 yaani ligi ya mabingwa na Europa league itakuja na sura mpya kukiwa na ongezeko la mechi mbili zaidi huku ile inayosimamiwa na FIFA kama kombe la dunia la vilabu sasa itakuja na sura mpya itakayoshirikisha timu 32 kutoka kuchukua bingwa wa ligi ya mabingwa kutoka kila bara.

Liverpool watakuwa wageni wa AC Milan katika dimba la Stadio Giuseppe Meazza jijini Milan kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya majira ya saa 4 usiku Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button