Nyumbani
Cadena apewa ‘Welcome’ Simba
ALIYEKUWA Kocha wa magolikipa wa klabu ya Azam, Daniel Cadena Ledesma ametambulishwa kuhudumia katika timu ya Simba.
Azam ilimpa ‘Thank You’ Cadena tarehe 14 mwezi uliopita.
Katika taarifa yake Simba imeandika: “Karibu Simba SC Kocha mpya wa Magolikipa, Daniel Cadena Ledesma.”
Wakati huo huo timu ya Azam imeshusha kocha mpya wa viungo.

“Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na Jean-Laurent Geronimi, atakayekuwa Kocha wetu wa viungo kuanzia msimu ujao 2023/24,” imesema Azam katika taarifa.
Geronimi anachakua nafasi ya Moadh Hiraoui aliyepewa ‘Thank You’ siku moja na Cadena.




