Nyumbani

Ki aapa kuwaliza Tarehe 8

DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameweka wazi nia yake ya kutaka kuharibu furaha za wapinzani wao katika mchezo wa Ngao ya Hisani utakaochezwa Alhamisi ya Agosti 8, mwaka huu.

Amesema sherehe imepita na wameingia kazini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ujao kukabiliana na mpinzani wao Simba uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Yanga juzi wamemaliza jambo lao la siku wananchi kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mabingwa wapya wa CECAFA Kagame cup 2024, Red Arrows ya Zambia na ku shinda mabao 2 – 1.

“Tumemaliza sherehe, baada ya mchezo dhidi ya Red Arrows ilikuwa sehemu ya maandalizi ya mchezo ujao, kwa sasa tunaangalia kile kinachofuata mbele yetu, msimu uliopita tulicheza nao Ngao ya Jamii tukapoteza.

Hatutaki kurudia makosa hayo, tumeanza maandalizi ili kufanya vizuri na kutwaa taji hilo na kuendeleza kile tulichoishia msimu uliopita,” amesema kiungo huyo wa Yanga.

Amesema mechi ya Red Arrows na mashindano ya kombe la Toyota nchini Afrika Kusini imewapa mwanga mzuri wa kujiandaa na msimu mpya na kupambana kutetea mataji yao na kufanya vizuri katika mchezo uliopo mbele yao dhidi ya Simba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button