Ligi Ya WanawakeNyumbani

Yanga Princess dimbani SLWPL leo

LIGI Kuu ya soka la Wanawake Tanzania Bara(SPWPL) inaendelea leo kwa michezo mitatu.

Yanga Princess itakuwa mwenyeji wa Amani Queens kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwenye uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu mkoani Arusha Fountain Gate Princess ni wageni wa wa The Tigers Queens.

Nao Baobab Queens ni wenyeji wa Alliance Girls kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Yanga Princess ipo nafasi ya 3 katika msimamo wa SLWPL ikiwa na pointi 17 baada ya michezo 8 wakati Amani Queens ni ya 9 ikiwa na pointi 4.

Alliance Girls inashika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 8 huku Baobab Queens ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 7.

Related Articles

Back to top button