Kwingineko

Pochettino awataka wachezaji United kuongeza umakini

LISBON: MAURICIO Pochettino ametoa wito kwa kikosi chake cha Manchester United kuboresha umakini wao, kufuatia makosa ya wachezaji mmoja mmoja yaliyosababisha timu hiyo kupoteza pointi tatu dhidi ya Sporting Lisbon.

Mwanzo mgumu wa kocha huyo raia wa Argentina akiwa na United uliendelea katika mechi yake hiyo ya pili, ambapo United ililazimishwa sare ya kusisimua ya mabao 2-2.

United ilisababisha penalti mbili katika kipindi cha kwanza, moja ikiokolewa, huku kipa Senne Lammens akidondosha mpira na kuwapa wenyeji bao la pili la kusawazisha dakika za mwisho.

Aidha, Youri Tielemans alioneshwa kadi nyekundu katika muda wa majeruhi wa kipindi cha pili baada ya kupokea kadi mbili za njano.

Alipoulizwa ni kwa namna gani wanaweza kuzuia makosa ya aina hiyo, aliiambia TNT Sports: “Katika hali kama hii, kama ilivyo katika klabu nyingine, tunahitaji kuwa bora zaidi. Tunahitaji kuzingatia zaidi, kuwa makini zaidi, na kujitahidi kurejesha hali zetu vizuri zaidi kwa kuweka juhudi zote.”

“Lakini tumeanza kurekebisha mambo. Kiwango kama cha leo (jana) ndiyo dawa bora ya kujiandaa kwa ajili ya mchezo ujao.

“Tumeonesha mtindo wa soka tunaotaka kuucheza. Tumekuwa pamoja kwa wiki moja tu.”

Baada ya mechi hiyo ya Ligi ya UEFA, United sasa inajipanga kukipiga na Brentford keshokutwa katika mwendelezo wa Ligi Kuu England.

“Kipaumbele ni mchezo unaofuata. Tunahitaji kuamini zaidi na zaidi. Katika kipindi cha pili, tulifanikiwa kurejesha mipira mingi katika nusu ya uwanja ya wapinzani. Huo ndio mtindo tunaotaka kuutumia.

“Tunahitaji kwenda Old Trafford, kuonyesha kujitolea, na kucheza kwa namna ileile tuliyoonesha dhidi ya Lisbon.”

Related Articles

Back to top button