Nyumbani

21 Serengeti boys kwenda Kombe la Dunia

DUBAI: KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Elieneza Nsanganzelu, ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kitakachoiwakilisha Tanzania katika fainali za Kombe la Dunia kwa vijana wa umri huo zitakazofanyika Qatar mwaka huu.

Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji kutoka klabu mbalimbali za ndani pamoja na mmoja anayekipiga nje ya nchi, Soann Adam Juma, anayeichezea Grenoble Foot 38 ya Ufaransa.

Klabu za Azam FC, Simba SC, Young Africans, KMC FC, JKT Tanzania, Fountain Gate FC, Kagera Sugar, Dodoma Jiji na KMKM ya Zanzibar pia zinawakilishwa katika kikosi hicho, huku wachezaji wengine wakitokea Kituo cha TDS.

Wachezaji waliochaguliwa ni Shaban Juma, Abrahman Nassoro (Azam FC), Haji Abdalah (TDS), Mohammed Ali (KMKM FC), Kassim Juma (TDS), Abubakar Othman (Young Africans), Hussein AMbeg (Simba SC), Soann Adam Juma (Grenoble Foot 38, Ufaransa), Abel Samson (JKT Tanzania), Issa Chole (Fountain Gate FC) na Juma Sagwe (KMC FC).

Wengine ni Luqman Mbalasalu (Kagera Sugar), Razaki J Mbegelendi (TDS), Elick Yusuph (TDS), Idrisa Kilendemo (TDS), Dismas Athanasi (TDS), Kelvin Revokatus (KMC FC), Hamis Mihambo (TDS), Sadam Hamis (TDS), Faraji Kayanda (Dodoma Jiji) na Bashiri Kibaila (Simba SC).

Serengeti Boys inatarajia kutumia fainali hizo kupima uwezo wake dhidi ya timu bora za vijana duniani, ikiwa ni hatua muhimu kwa maendeleo ya soka la vijana nchini na kuwapa wachezaji nafasi ya kujitangaza katika jukwaa la kimataifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button