Nyumbani

Simba mikononi mwa Mo Dewji tena

DAR ES SALAAM: ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again ‘, ametangaza rasmi kuachia nafasi yake huku Simba ikitarajia kurejea mikononi wa Mwekezaji Mohammed Dewji.

Ameyasema hayo alipofanya mahojiano maalum na Azam TV, Try Again amesem kipindi cha mpito ambacho wamekipitia kwa miaka mitatu na bila kufikia malengo yanayotarajiwa ameona bora kuachia ngazi.

Amesema wana wajibu mkubwa wa kusaidia Simba kurejesha heshima yake kwa baadhi ya viongozi kutangaza kujiuzulu na kupisha wengine kuja kuiondoa hapo ilipo ikiwemo kutwaa mataji ambayo yalipotoa mwa miaka mitatu.

“Baada ya kutamatika kwa msimu huu nilienda kukutana na Mo Dewji kumkabidhi ripoti na tathimini ya timu yetu ya wapi tulipokosea na kutakiwa kufanyia maboresho, nimemuomba kuja kuchukuwa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi na kuirejesha Simba katika ubora wake,” amesema Try Again.

Amesema anatoka katika nafasi hiyo kupisha uimarishaji wa klabu hiyo ambayo kwa misimu takribani mitatu ya karibuni timu hiyo kuwa na mzoroto wa matokeo hali iliyoibua hali ya mchafukoge kwa takribani majuma mawili klabuni humo.

Try Again amesema anamshukuru Mwekezaji huyo kuwa bega kwa bega kwa miaka saba ambayo amekuwa ndani ya Simba na anaimani na Usimba wa Mo Dewji kuivusha timu hiyo katika kipindi kigumu ambacho kimepita sasa.

Kuhusu usajili, amesema ni suala la bahati nasibu, dirisha kubwa walileta wachezaji wapya watano Ayoub Lakred, Fabrice Ngoma, Luis Miquissone, Fondoh Chemalone ambao wote wamefanya vizuri kasoro Aubin Kramo ambaye alipata majeraha.

“Katika dirisha dogo amekuja Omar Pa Jobe na Fred Michael ameweza kuingia katika mfumo na kumaliza ligi akiwa na mabao 10 na anaongoza ufungaji bora Zambia alipokuwa akicheza kabla ya kusajiliwa Simba,” ameelezea.

Try Again ameongeza kuwa suala la kocha wanalazimika kuwaondoka kwa sababu ya kutofikia malengo yao hasa kwa miaka mitatu ambayo hatukuwa sawa na kupoteza mataji.

Related Articles

Back to top button