Nyumbani

Simu ya usiku iliyomfikisha Bakari Msimu Simba

DAR ES SALAAM: WINGA mpya wa kulia wa Simba Bakari Msimu amesema hakutarajia kabisa kupata nafasi ya kujiunga na Simba SC, akieleza kuwa kila kitu kilianza baada ya mchezo kati ya Coastal Union na Simba uliomalizika kwa ushindi wa Wekundu wa Msimbazi wa mabao 2-1.

Msimu amesema baada ya kurejea kambini na kumaliza chakula cha usiku, alipigiwa simu na mtu aliyemwambia akafike sehemu fulani kwa mazungumzo muhimu. Alipofika, alipewa taarifa iliyombadilishia maisha yake ya soka.

“Nilikuwa kambini baada ya mechi. Nikapigiwa simu na nikaambiwa kuna mtu ananitafuta. Nilipofika nikaelezwa kuwa viongozi wa Simba wananihitaji. Kwangu ilikuwa ni ‘surprise’ kubwa, lakini pia ndoto ya kila mchezaji kupata nafasi ya kuchezea klabu kubwa kama Simba,” amesema Msimu katika mahojiano maalum.

Ameongeza kuwa hata kabla ya kusaini mkataba, tayari baadhi ya mashabiki wa Simba walikuwa wakimkaribisha na kumtakia mafanikio, jambo lililompa hamasa zaidi ya kuanza safari mpya ya soka.

Msimu amesema anafahamu matarajio makubwa ya mashabiki wa Simba na ameahidi kujituma kwa bidii ili kuchangia mafanikio ya timu hiyo msimu ujao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button