Afrika Mashariki

Asha Djafari ajiunga na Gokulam Kerala

NEW DELHI: KIUNGO wa kimataifa wa Burundi, Asha Djafari amejiunga na klabu ya Gokulam Kerala FC ya India baada ya kuitumikia Yanga Princess msimu uliopita, akianza safari mpya ya soka katika Ligi ya Wanawake ya India (IWL).

Asha, ambaye pia aliwahi kucheza Simba Queens, anarejea kucheza soka nje ya Tanzania akiwa na uzoefu wa mashindano ya ndani na ya kimataifa.

Klabu ya Gokulam Kerala FC imemtangaza mchezaji huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, ikieleza kuwa kiungo huyo wa Burundi ana uzoefu muhimu wa mashindano ya ngazi ya juu nchini Tanzania na katika maeneo mbalimbali ya Afrika.

Katika taarifa yake ya kumkaribisha, klabu hiyo imeeleza kuwa inafurahia kumpokea Asha na kutarajia kutumia uzoefu wake katika kuimarisha kikosi hicho kuelekea mashindano ya msimu.

Usajili huo unampa Asha nafasi ya kuendeleza kipaji chake katika soka la wanawake nchini India, huku akitarajiwa kuleta mchango muhimu kutokana na uzoefu alioupata akiwa na klabu za Simba Queens na Yanga Princess nchini Tanzania.

IHatua hiyo pia ni fursa kwa kiungo huyo wa Burundi kuendelea kujijengea jina katika soka la kimataifa kupitia mashindano ya Ligi ya Wanawake ya India.

Related Articles

Back to top button