Kwingineko

Kane aandika historia England afikisha mechi 125

LONDON, Uingereza: NAHODHA wa England, Harry Kane, amekuwa na usiku wa kihistoria baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Czech Republic kwenye Uwanja wa Wembley.

Kane alifunga mabao mawili katika mchezo huo, akifikisha idadi ya mechi alizoichezea England kuwa 125, sawa na rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mlinda mlango wa zamani wa timu hiyo, Peter Shilton.

Ushindi huo ulimpa Kane nafasi ya kuendelea kuweka historia katika kikosi cha England, huku akiwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi katika kizazi cha sasa cha timu hiyo.

Kocha wa England, Thomas Tuchel, alimpongeza Kane kwa mchango wake katika ushindi huo, akisisitiza kuwa mshambuliaji huyo wa Bayern Munich alistahili heshima na sifa zote kutokana na hatua hiyo kubwa.

Tuchel alisema Kane alikuwa muhimu kwa England katika mchezo huo, akieleza kuwa siku hiyo ilikuwa ya kipekee kwake kutokana na kufikia rekodi ya mechi 125 akiwa na taifa lake.

“Alikuwa, tena, muhimu sana kwetu katika siku hii ambayo ilikuwa ya kipekee kwake,” alisema Tuchel, huku Kane akiendelea kuandika historia katika timu ya taifa ya England.

Related Articles

Back to top button