AFCON

Shime aomba radhi baada ya Twiga kuaga WAFCON

CANSABLANCA: KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Bakari Shime, amewaomba radhi na kuwapa pole mashabiki pamoja na Watanzania waliokuwa na matumaini ya kuona timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ikiendelea na safari yake kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026.

Twiga Stars iliondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Ivory Coast kwa mabao 2-1, matokeo yaliyomaliza matumaini ya Tanzania kusonga mbele.

Shime amesema kikosi chake kilikuwa na malengo ya kufanya vizuri katika michuano hiyo, lakini kwa bahati mbaya hakikuweza kufikia matarajio yaliyowekwa.

“Tunawaomba radhi Watanzania na mashabiki wetu wote waliokuwa nyuma yetu. Tulikuwa na malengo makubwa, lakini mambo hayakwenda kama tulivyotarajia,” amesema Shime.

Kocha huyo amesema kuondoka kwenye mashindano hayo ni sehemu ya safari ya kujifunza na kujenga timu, huku akiahidi kuwa benchi la ufundi litafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.

Amesema uzoefu walioupata kwenye WAFCON utasaidia kufanya maboresho kuelekea mashindano yajayo na kuhakikisha Twiga Stars inaendelea kuwa na ushindani zaidi katika ngazi ya kimataifa.

Related Articles

Back to top button