Klopp: Tulizunguka na Mbappe kwenye ndege, kisha akaenda PSG

BOSTON: BAADA ya mechi ya usiku wa kuamkia leo ambayo Ufaransa iliikunyuga Morocco mabao 2-0, Kylian Mbappe alikuwa na kocha Jurgen Klopp wakionesha kidole jukwaani na kucheka.
Kicheko hicho nyuma yake kina stori kubwa kwani walikuwa wakionyeshana mama yake Mbappe, Fayza na kukumbuka mwaka 2017 Liverpool ilipotaka kumsajili nahodha huyo wa Ufaransa na kugonga mwamba.
“Nilizungumza na Liverpool, klabu pendwa ya mama yangu, anaipenda sana hii timu,” alianza kueleza Mbappe kilichotokea mwaka huo wakati akiwa na AS Monaco kisha Klopp aliyekuwa kocha wa Liverpool wakati huo kumalizia mkasa mzima.
“Hii ilikuwa ni gharama kubwa zaidi tuliyotumia kwa ajili ya usajili ambao haukufanikiwa.
“Tuliruka kutoka Blackpool kwenda Nice. Huko Nice, familia nzima ya Mbappé ilipanda ndege binafsi iliyokuwa na vyumba vitano au zaidi.
“Ilikuwa ndege kubwa sana. Tulifanya jambo kubwa kweli. Tukaruka angani kwa kuzunguka-zunguka, tukazungumza na familia hiyo na tukala chakula kizuri.
“Yote haya yalifanyika ndani ya ndege. Hatukuruhusiwa kuonekana. Hivyo tukaruka kwa kuzunguka, tukala, tukawa na wakati mzuri kakini mwisho wa siku (Mbappe) akaenda Paris.”
Aidha, katika mechi hiyo, Mbappe ambaye kwa sasa ni staa wa Real Madrid alifunga bao moja na kuipelekea Ufaransa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2026.




