Muziki

Ray C: Msiite msanii wa zamani, mlichelewa kuja mjini

MSABNII wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, amesema hataki kuitwa msanii wa zamani au mkongwe, akieleza kuwa matumizi ya kauli hiyo hayampi heshima anayostahili na mara nyingi hutumiwa na watu walioingia kwenye tasnia ya muziki baadaye.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Ray C alisema anapinga tabia ya baadhi ya mashabiki na wadau wa muziki kuwatambulisha baadhi ya wasanii kama wa zamani, akisisitiza kuwa muziki wao bado una mchango mkubwa katika tasnia.

“Biashara ya kuitana msanii wa zamani mnitue, na Remmy Ongala mtasema wa lini? King Kiki je? Bi Kidude wa Mtondogo au? Semeni tu mlichelewa kuja mjini ndiyo nishajiamulia,” ameandika Ray C.

Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki wa muziki, huku baadhi wakiunga mkono msimamo wake kwamba wasanii waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Bongo Fleva wanapaswa kuthaminiwa kwa kazi zao badala ya kutambulishwa kwa misamiati inayoweza kuonekana kuwadunisha.

Related Articles

Back to top button