Nyumbani

Simba yaingia Zanzibar kibabe

ZANZIBAR: KIKOSI cha Simba kimewaili visiwani Zanzibar tayari kwa michuano ya Kombe la Muungano huku wakiahidi kuendelea kutoa burudani katika mchezo dhidi ya Mafunzo FC utakaochezwa kesho.

Kwa mujibu wa Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, wamejipanga kuendelea kuhamishia burudani kwa mashabiki wao wa Zanzibar na kuhakikisha wanafanya vizuri katika hatua zote.

Amesema michuano hiyo ni nafasi ya kipekee kwa wachezaji waliokuwa hawapati nafasi kuonesha vipaji vyao.

“Tumejipanga kwenda kutoa burudani kwa mashabiki wetu wa Zanzibar, kesho tuna mchezo muhimu na melengo niu kushinda kila hatua, benchi la ufundi limejipanga vizuri na wachezaji wote wako imara,”amesema.

Michuano ya Kombe la Muungano hukutanisha timu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na umoja lakini pia, ushindani wa soka nchini.

Related Articles

Back to top button