Ligi Kuu

Mbeya City siyo kinyonge dhidi ya Yanga

DAR ES SALAAM: WAKATI presha ikizidi kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa KMC, mabosi na wachezaji wa Mbeya City wameweka wazi dhamira yao ya kusaka ushindi bila kuyumba.

Ofisa Habari wa Mbeya City, Gwamaka Mwankota, amesema kelele zinazoendelea nje ya uwanja haziwatishi, badala yake zimewapa ari zaidi ya kupambana.

“Tumekuwa tukisikia milio mingi, wengine wakisema tumetumwa, lakini sisi si bundi wala paka. Ni kweli tumetumwa, lakini tumetumwa na wananchi wa Mbeya wanaotuamini kwenda kufanya kazi yao – kusaka pointi tatu,” amesema Mwankota.

Kwa upande wake, mshambuliaji wa timu hiyo, Eliud Ambokile, amesema wanatambua ugumu wa mchezo huo hasa wakijua Yanga wanahitaji matokeo, lakini nao wamejiandaa ipasavyo.

“Tunajua Yanga wanahitaji matokeo katika mechi hii. Kule nyumbani tulipata sare, hivyo watakuwa wanaitaka sana mechi hii. Tunawaheshimu, lakini na sisi tunazitaka hizo pointi tatu,” amesema Ambokile.

Ameongeza kuwa morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja yupo tayari kupambana kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

Mbeya City inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya sare katika mchezo wa kwanza, huku Yanga wakisaka ushindi ili kujiimarisha zaidi kwenye msimamo wa ligi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button