BASATA yamuita Halima Haji

DAR ES SALAAM: BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limemuita msanii Halima Haji pamoja na meneja wake, Rahma Pascal, kufuatia kusambaa kwa kipande cha video ya muziki kinachodaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na BASATA, kikao hicho ambapo wahusika walifika mbele ya Baraza na kukiri kufanya kosa hilo.
Kufuatia kukiri huko, BASATA imesema kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa kulingana na taratibu na sheria zilizopo.
Baraza hilo limeeleza kuwa litaendelea kusimamia kwa karibu maudhui ya kazi za sanaa nchini, likilenga kuhakikisha kuwa yanazingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania.
Aidha, BASATA imetoa onyo kali kwa wasanii wote nchini kuwa haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote atakayebainika kukiuka miongozo na kanuni zilizowekwa.




