Ligi Kuu

Pedro awapa tano wachezaji wake

SINGIDA: KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, ameipongeza timu yake kwa kuonesha kujituma na kujitoa kwa kiwango kikubwa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida Black Stars.

Akizungumza baada ya mchezo huo wa Ligi Kuu uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Airtel jana, Goncalves amesema kikosi chake kilionesha nidhamu, kujitoa na umoja mkubwa uwanjani hali iliyowasaidia kupata ushindi huo muhimu.

Amesema ushindi huo unaendelea kuiweka timu hiyo kileleni mwa msimamo wa ligi huku ikiwa na safu bora ya ushambuliaji pamoja na ulinzi imara msimu huu.

Yanga inaongoza kwa pointi 30 katika michezo 12, ikiwa imefunga mabao 30, mengi kuliko timu nyingine na ndio timu pekee iliyoruhusu mabao machache kwenye nyavu zake yaani mawili.

“Ulikuwa mchezo mzuri sana kutoka kwa timu. Wachezaji wameonesha kujitoa na kujituma kwa kiwango kikubwa,” amesema Goncalves.

Yanga sasa inaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa Jumapili.

 

Related Articles

Back to top button