Dulla Makabila akanusha mahusiano na mama wa Hamisa Mobetto

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo Fleva, Dulla Makabila, ameibuka na kuvunja ukimya kuhusu taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zikimdai aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama wa Hamisa Mobetto.
Dulla amesema amewahi kusikia tetesi hizo lakini hazina ukweli wowote, akisisitiza kuwa anamuheshimu sana mama mzazi wa Hamisa na hawezi kufanya jambo la namna hiyo.
“Nilisikia bwana, niliwahi kusikia. Sijui ilitokea wapi hiyo skendo. Yule mtu namuheshimu sana, siwezi kufanya hivyo. Mmenikosea sana kwa mara ya kwanza, waandishi,” amesema Dulla alipokuwa kwenye mashindano ya Ramadhan Cup, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa uvumi huo ulimshangaza na hata kumuumiza, kwa sababu unaweza kuharibu heshima na mahusiano ya watu bila sababu ya msingi.
Kwa mujibu wa Dulla, anathamini sana maadili na heshima yake, na hana sababu ya kujiingiza katika jambo litakaloweza kuleta tafsiri potofu katika jamii.




