Ligi Kuu

Ibenge awapa heko wachezaji wake

DAR ES SALAAM : KOCHA Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema ameridhishwa na ushindi wa mabao 3-0 walioupata dhidi ya Mtibwa Sugar jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Ibenge amewapongeza wachezaji wake kwa kutengeneza nafasi nyingi na kucheza soka la kuvutia.

Aidha, Ibenge amesema timu yake imeonesha uimara mkubwa kwa kufunga mabao matatu bila kuruhusu bao, jambo linaloonesha maendeleo mazuri ya kikosi hicho katika mechi za hivi karibuni.

“Hongera kwa wachezaji kwa sababu wametengeneza nafasi nyingi, wamefunga mabao matatu na hawajaruhusu kufungwa. Tuna furaha kwa kupata pointi tatu na kucheza soka zuri,” amesema.

Kocha huyo pia amewapongeza mashabiki kwa kuendelea kuwa nyuma ya timu hiyo na kusisitiza umuhimu wao katika michezo ijayo.

Amesema sasa wanaenda Mwanza ambapo watacheza michezo miwili akitarajia kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki watakaosafiri kwenda kuiunga mkono timu hiyo.

Related Articles

Back to top button