Ligi Kuu

Chasambi awapigia magoti Simba

DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Simba, Ladack Chasambi amewaomba radhi viongozi,  wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwakosesha alama tatu dhidi ya Fountain Gate FC.

Katika maelezo yake kupitia ukurasa wake wa mitandano ya kijamii, Chasambi amesema anapenda kuchukuwa fursa kuomba radhi  kwa uongozi wa klabu, benchi la ufundi, wachezaji wenzangu, na zaidi ya yote, mashabiki na wapenzi wa Simba kutokana na makosa aliyofanya kugharimu timu hiyo.

“Najua jinsi mnavyoipenda na kuiunga mkono klabu hii kwa moyo wote, ninaelewa matokeo yoyote yanayoiumiza timu, huwaumiza ninyi kama familia yetu.

“Sikutamani kabisa kufanya kosa hilo, lakini ni sehemu ya mchezo najifunza kutokana na hali hii kuwa mchezaji bora zaidi kwa ajili yenu na timu,” amesema.

Chasambi amesema anaahidi kujituma zaidi, kujifunza kutokana na makosa, anarejea akiwa na ari mpya ya kupigania mafanikio ya klabu ya Simba.

“Naahidi kujituma zaidi, naomba radhi kwa yeyote aliyeumizwa na kitendo changu, naomba muendelee kuniamini na kuniunga mkono,”amesema.

Related Articles

Back to top button