Kwingineko

Uwoya: “Usinichokoze, siongei ngumi zinaruka!”

DAR ES SALAAM :MSANII wa filamu za Bongo Movie, Irene Uwoya, amesema kuwa huwa hapendi kukaa kimya anapokasirishwa, akieleza kuwa hasira zake ziko karibu na mara nyingi huishia kutumia nguvu pale anapochokozwa kupitiliza.

Akizungumza kuhusu tabia yake, Uwoya amesema kuwa si mtu wa kubishana kwa maneno kwa muda mrefu, kwani akishajibiwa mara kadhaa hushindwa kuendelea kuongea na badala yake ngumi zinaweza kuhusika.

“No, nina hasira za karibu. Yaani ukinipa neno la kwanza nikakujibu, la tatu ukinijibu siwezi kuongea kwa sababu kuongea sijui, yani hapo itatokea ni ngumi tu,” amesema Uwoya.

Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki wake, wengi wakieleza kushangazwa na ukiri huo wa wazi kuhusu namna anavyokabiliana na hasira.

Uwoya ni miongoni mwa wasanii waliodumu kwa muda mrefu kwenye tasnia ya filamu nchini, akijizolea umaarufu mkubwa kupitia kazi zake mbalimbali za uigizaji.

Hata hivyo, kupitia kauli yake hiyo, amewataka watu kujiepusha na kumchokoza mara kwa mara kwani hasira zake zinaweza kumpelekea kuchukua hatua za haraka.

Related Articles

Back to top button