Mastaa

Vera Sidika:Nawapenda wanaume wa Tanzania

'wanapendelea vitendo xaidi kuliko maneno'

DAR ES SALAAM:MWANAMITANDAO maarufu kutoka nchini Kenya, Vera Sidika, amesema kuwa anavutiwa zaidi na wanaume wa Tanzania akieleza kuwa wanapendelea vitendo kuliko maneno mengi.
Vera, ambaye kwa sasa yupo California, Marekani, ameyasema hayo kupitia mahojiano aliyofanya na Vidyfy_us chini Jacchalz.

Katika mahojiano hayo, Vera ameweka wazi kuwa kwa sasa yupo single.
Hata hivyo, alibainisha kuwa hali yake ya mahusiano inategemea na mtu atakayemuuliza swali hilo, akimaanisha kuwa yuko wazi kwa uwezekano wa kuwa kwenye uhusiano endapo atampata mtu sahihi.

Akizungumzia aina ya mwanaume anayevutiwa naye, Vera amesema anapenda wanaume wapole, wanaochukua hatua na kuonyesha mapenzi kwa vitendo badala ya kuishia kwenye maneno matamu pekee.

Aidha, amesisitiza kuwa ana mapenzi ya kipekee kwa wanaume wa Tanzania, akidai kuwa ni wazuri na wana sifa anazozipenda. Vera alifichua kuwa aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kutoka Tanzania, lakini hakutaka kuweka wazi jina lake.

Kauli hiyo imeibua mjadala mtandaoni, huku mashabiki wake wakionesha hisia tofauti kuhusu mapendeleo yake hayo.

Related Articles

Back to top button