Tuzo ya Walk of Fame 2025 kupewa aliyefariki akiwa na miaka 101
NEW YORK: MUIGIZAJI na mwanaharakati Toni Vaz ambaye anatarajiwa kutunukiwa na nyota kwenye Hollywood Walk of Fame mwakani 2025, amefariki akiwa na umri wa miaka 101.
Vaz aliyefariki dunia katika chuo cha Motion Picture Fund huko Woodland Hills, Calif mnamo Oktoba 4 mwaka huu. Alikulia katika Jiji la New York na ndugu zake wanne na wazazi wake, ambao walihamia kutoka Barbados, Variety iliripoti. Alipokua na kuamua kuendelea na kazi yake ya uigizaji, Vaz alihamia Hollywood na kufanya shughuli za matamasha kama ziada katika filamu ya 1959 ‘Tarzan’ na ‘the Ape Man’.
Vaz pia alidhamiria kufungua fursa zaidi kwa waigizaji Weusi. Alianzisha Tuzo za Picha za NAACP. Tuzo hizo zinazowaheshimu watu wa rangi tofauti zilifanya sherehe yake ya kwanza Agosti 13, 1967.
Mnamo 2021, Vaz alipokea Tuzo la Waanzilishi wa Tuzo za Picha. Mwigizaji Yvette Nicole Brown alianzisha Tuzo ya Mwanzilishi na kuelezea Vaz kama ‘mvumbuzi wa kweli Mweusi.’
“Wakati ambapo kulikuwa na nafasi ndogo sana za vipaji vya watu weusi huko Hollywood, aliweka mtazamo wa kubadilisha Waamerika wa Kiafrika katika tasnia ya burudani ndipo Tuzo za Picha za NAACP zikaanzishwa.”
Vaz alizungumza kwa fahari juu ya maendeleo ya Hollywood wakati Baraza la Jiji la Las Vegas lilipoheshimu Chama cha Watu Weusi mnamo 2006.