Filamu

Star wa filamu ya Apocalypto Gerardo Taracena, afariki dunia

MEXICO: TASNIA ya filamu na sanaa ya maigizo nchini Mexico imekumbwa na pigo kubwa baada ya kifo CHA mmoja wa waigizaji wa fiamu ya Apocalypto iliyotoka mwaka 2006, Gerardo Taracena, kufariki dunia.

Muigizaji huyo na densa maarufu nchini humo amefariki akiwa na umri wa miaka 55.

Awali hawakutoa maelezo rasmi kuhusu sababu ya kifo, lakini wakati wa mazishi, rafiki yake Enrique Cueva alisema kwamba Taracena alikuwa na shinikizo la damu (hypertension) na aligundua moyo ndiyouliosababisha kifo chake.

Hadi sasa, hakujatangazwa rasmi tarehe halisi ya mazishi ya Gerardo Taracena katika taarifa za umma, na maelezo ya mazishi yanategemea taarifa rasmi zaidi kutoka kwa familia au wawakilishi wake ikiwa itaenda hadharani baadaye.

Taracena amezaliwa Machi 27, 1970, jijini Mexico, alianza mapema kuvutiwa na sanaa ya maonesho. Alisomea sanaa ya uigizaji na pia kufundishwa densi, jambo lililomjengea nidhamu ya mwili, umakini na uwezo mkubwa wa kuwasilisha hisia kupitia vitendo.

Kabla ya kung’ara kimataifa, Taracena alishiriki katika zaidi ya maonesho 30 ya jukwaani, akiwa sehemu ya kundi la Theatre Myth, na kushiriki katika matamasha mbalimbali ya maigizo barani Amerika ya Kusini.

Umaarufu wake mkubwa ulianza mwaka 2006 kupitia filamu Apocalypto, iliyomfungulia milango ya kimataifa na kumtambulisha kama mmoja wa waigizaji hodari kutoka Mexico.

Baada ya Apocalypto, Taracena alipata nafasi katika filamu za kimataifa ikiwemo ‘The Mexican’ na ‘Man on Fire’, huku pia akiendelea kung’ara katika filamu za Mexico kama ‘The Violin’, ‘Sin Nombre’ na ‘Saving Private Perez.’

Related Articles

Back to top button