AfricaAfrika MasharikiCHAN

25 waitwa Taifa Stars, Kakolanya yumo

KIKOSI cha wachezaji 25 wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kitaingia kambini Agosti 21, 2022 kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.

Kikosi hicho kinajiandaa na mchezo dhidi ya Uganda utakaopigwa Agosti 28 uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kabla timu hizo kurudiana Septemba 3 uwanja wa St. Mary’s uliopo Entebbe, Uganda.

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars  Kim Poulsen amemjumuisha kwenye kikosi hicho kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya ikiwa ni miaka mitatu tangu alipocheza mara ya mwisho dhidi ya Burundi mwaka 2019.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Poulsen Dar es Salaam Poulsen amesema wachezaji aliowaita ni wale walikuwepo awali na baadhi ya nyota ambao wameongezwa katika kuimarisha kikosi kuelekea michezo hiyo.

“Wachezaji wengi walikuwepo katika mchezo uliopita dhidi ya Somalia lakini pia kuna baadhi nimewaita, tunahitaji kupata matokeo mazuri katika michezo hiyo miwili,” alisema Poulsen.

Amewataja wachezaji watakaoingia kambini kuwa ni Aishi Manula, Abutwalib Mshery, Kakolanya, Kibwana Shomari, Mohammed Hussein, Paschal Msindo, Nathan Chilambo,  Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Kennedy Juma, Sospeter Bajana na Jonas Mkude.

Wengine ni Mzamiru Yassin, Kelvin Nashon,  Feisal Salum, Farid Mussa, Abdul Seleman, Relliants Lusajo,  Kibu Denis, Habib Kyombo, George Mpole, Anwar Jabir, Danny Lyanga na Salum Abubakar.

Related Articles

Back to top button