
DAR ES SALAAM: MSANII wa filamu nchini, Zaiylissa, amefafanua kuwa ndoa yake ya sasa bado ipo, huku akieleza kuwa ushiriki wake katika video ya wimbo mpya wa msanii wa Singeli, Dulla Makabila, ulipata baraka kutoka kwa mume wake wa sasa.
Zaiylissa amesema kuonekana kwake katika video hiyo haikuwa uamuzi wake pekee, bali mume wake alifahamu na kuridhia ushiriki wake katika kazi hiyo.
Akizungumzia kuhusu suala hilo, mwigizaji huyo ameeleza kuwa Dulla Makabila ndiye aliyemwomba ruhusa mume wake ili Zaiylissa aweze kushiriki katika video ya wimbo huo, na mume wake alikubali.
Kwa upande mwingine, Zaiylissa amesema mume wake wa sasa, ambaye si msanii, anaelewa vyema mazingira ya kazi yake ambayo yanahusisha sanaa.
Kwa sababu hiyo, anafahamu kuwa kushirikiana na wasanii wengine ni sehemu muhimu ya shughuli zake za kikazi.
Aidha, Zaiylissa amesema mume wake humpa uhuru wa kutosha kufanya kazi na shughuli mbalimbali za maendeleo, badala ya kukaa nyumbani muda wote bila kujishughulisha.
Ikumbukwe kuwa Zaiylissa na Dulla Makabila waliwahi kuwa katika ndoa kabla ya kutengana na kila mmoja kuendelea na maisha yake binafsi.




