Burudani

Steve Mweusi awataka wachekeshaji kuwa wabunifu

WASANII wanaofanya sanaa mbalimbali nchini wametakiwa kuwa wabunifu na hivyo kuwezesha kiurahisi kupata soko kwa jamii inayowaburudisha.

Wito huo umetolewa na mchekeshaji maarufu nchini Steve Moses maarufu ‘Steve Mweusi’ alipozungumza na SpotiLEO kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa mtandao huu.

“Hii ndio kazi tuliyoichagua pia juhudi ni muhimu tujitahidi kuwa wabunifu kwa sababu watu wanatuamini na sisi tusiwapoteze,” amesema Steve.

Katika upande mwingine, Steve ambaye ana miaka saba ya sanaa ya uchekeshaji amesema katika kuhakikisha anatanua wigo wa kazi zake kimataifa amepanga kufanya kazi na baadhi ya wachekeshaji katika baadhi ya mataifa Afrika.

“Nina mialiko zaidi ya 10 kwa hiyo mwaka huu kuanzia mwezi wa saba naanza ziara nikianza Kenya, DR Congo na baadaye Marekani na kwingineko,” ameongeza Steve.

Related Articles

Back to top button