Tuzo za wachekeshaji kuzinduliwa

DAR ES SALAAM: BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania leo linatarajia kuzindua rasmi Tuzo za Wachekeshaji Tanzania zinazotarajia kufanyika Februari 14, 2025, katika ukumbi wa The Super Dome.
Akizungumza na Spoti leo Katibu Mtendaji wa BASATA, Dk Kedmon Mapana, amesema tuzo hizi ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita,katika kukuza na kuthamini mchango wa wasanii wa comedi.
“Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuthamini mchango wa wachekeshaji katika kukuza sanaa na kuendeleza vipaji tunazindua rasmi tuzo za wachekeshaji.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dk Gervas Kasiga, amesema wachekeshaji ni mabalozi muhimu wa taifa letu, wakichangia kueneza utamaduni na kuinua hadhi ya Tanzania katika anga za kimataifa.
“Leo Usiku vitatangzwa vipengele mbalimbali vya tuzo hizi, ikiwemo Comedian of the Month, Comedian of the year, Female Comedian, vimetangazwa katika katika uzinduzi huo.
“Wasanii na wadau wa sanaa wameombwa kushiriki kwa wingi na kuzitangaza tuzo hizi kwa ubunifu, ili kuhamasisha ushirikiano na kuungwa mkono na Watanzania wote.
“Tuzo hizi ni hatua kubwa ya kuenzi juhudi za wachekeshaji na kuimarisha sekta ya burudani nchini. Usikose kushiriki na kuwa sehemu ya historia! kubwa kwa wachekeshaji nchini.”amesema Kasiga