Ligi Kuu

Yanga kuivaa Coastal kwa tahadhari

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, amesema wanatambua ubora wa Coastal Union na wamejipanga kwa umakini kukabiliana na timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam leo kueleeka katika mchezo huo , Mngqithi amesema Coastal Union ni timu yenye ushindani mkubwa, huku akibainisha kuwa wamefanya uchambuzi wa kikosi hicho na kufahamu maeneo ambayo kina nguvu.

“Coastal Union ni timu ambayo tunapaswa kuwa nayo makini sana. Nimemtazama kipa wao Juma, mabeki wao wa kati si wabaya, pamoja na viungo wao wa kati, Godfrey na Ally, ambao walicheza vizuri katika mchezo uliopita.

“Ni timu yenye ushindani mkubwa. Wako vizuri kwenye mipira ya juu kwa sababu washambuliaji wao ni warefu. Tunajua tunakwenda kucheza na timu gani, na tunajua ubora walio nao,” amesema Mngqithi.

Kwa upande wake, Kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias, amesema wao pia wamewasoma Yanga na wanaamini mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.

Fikiri amesema wanakwenda kucheza dhidi ya kocha mwenye utambulisho wa wazi wa namna anavyotaka timu yake icheze, huku akieleza kuwa Yanga ina wachezaji wenye uwezo mkubwa.
Mwisho

Related Articles

Back to top button