Ligi Kuu

Dabi ni lazima wafunge mabao 2

JUMAMOSI Oktoba 19 Tanzania na Afrika itashuhudiwa moja ya Dabi kubwa ya kandanda Afrika ambapo klabu kubwa zaidi kwenye soka la Tanzania Simba na Yanga zitakipiga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo leo tunakusogezea baadhi ya mambo muhimu kuhusu timu, makocha na wachezaji waliowahi kucheza au wanacheza mpaka sasa kwenye klabu za Simba na Yanga.

Je unafahamu kwamba ni wachezaji watano pekee wamefunga mabao mawili kwenye mchezo mmoja uliozikutanisha Simba na Yanga tangu mwaka 2010?.
Wachezaji hao ni Mussa Mgosi aliyekipiga Simba, alifunga mabao hayo Aprili 2010.

Jerry Tegete wakati akikipiga Yanga alifunga mabao mawili timu hizo zilipokutana Aprili 2010.

Emmanuel Okwi wakati akikipiga Simba alifunga mabao mawili Mei 2012 Simba walipoichabanga Yanga mabao 5-0.

Hamis Kiiza enzi zake akiwa Yanga alifunga mabao mawili Oktoba 20, 2013 kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 3-3.

Maxi Nzengeli wa Yanga Novemba 05, 2023 alifunga mabao mawili kwenye mchezo Yanga walioshinda mabao 5-1.

Related Articles

Back to top button