Ligi KuuNyumbani

Meck Maxime ‘out’ Kagera Sugar

KLABU ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kagera Sugar imevunja mkataba na kocha wake Meck Maxime.

Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Mtendaji Mkuu, Ibrahim Mohamed imesema vile vile klabu hiyo imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo, Francis Mkanula.

“Klabu ya Kagera Sugar imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkabata na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Meck Maxime,’ imesema taarifa hiyo.

Kagera Sugar inayoshika nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 13 imesema katika kipindi cha mpito kikosi cha timu hiyo kitakuwa chini ya Kocha Marwa Chamberi.

Imesema tayari mchakato wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button