Yanga kuifuata Al Ahly leo
MSAFARA wa watu 60 wa klabu ya Yanga utaondoka leo jioni kwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa mwisho na wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Machi Mosi kwenye uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema hayo Dar es Salaam leo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi.
“Tutaondoka na msafara wa watu 60, msafara huu umegawanyika makundi matatu, wachezaji 24, benchi la ufundi 13, na watendaji/maofisa wakuu wa klabu 23,” amesema Kamwe.
Kikanuni tayari Yanga imefuzu hatua ya robo na mchezo dhidi ya Al Ahly utakuwa wa kukamilisha ratiba lakini Kamwe amesema lengo ni kushinda ili kuongoza kundi.
“Tunataka kuongoza kundi, ili tupate faida ya kuanza mchezo wetu wa robo fainali ugenini, tunataka kucheza na walioshika nafasi ya pili,” amesema.
Msimamo wa kundi D hadi sasa ni kama ifuayavyo:
# | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | 5 | 2 | 3 | 0 | 5 | 1 | 4 | 9 | |
2 | 5 | 2 | 2 | 1 | 9 | 5 | 4 | 8 | |
3 | 5 | 1 | 2 | 2 | 4 | 6 | -2 | 5 | |
4 | 5 | 1 | 1 | 3 | 3 | 9 | -6 | 4 |