AfricaKusini Mwa Afrika
Tanzania kutinga fainali COSAFA wanawake leo?

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake(Twiga Stars) leo itaikabili Zambia katika nusu fainali ya ubingwa wa Baraza la Vyama vya soka Kusini mwa Afrika(COSAFA) kwa wanawake.
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Isaak Wolfson ulipo jiji la Port Elizabeth, Afrika Kusini.
Twiga imetinga nusu fainali baada ya kuitoa Malawi kwa mabao 3-1.
Mshindi wa nusu fainali kati ya Tanzania na Zambia atacheza na mshindi wa nusu fainali nyingine kati ya Afrika Kusini na Namibia.