Africa

Kamwe: Hatuwezi kumdharau mpinzani

Afisa Habari Yanga Ally Kamwe amesema malengo ya klabu hiyo ni kufika mbali katika michuano ya kimataifa hivyo haiwezi kudharau timu pinzani.

Kamwe amesema hayo Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa marudiano wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asas Djibouti Agosti 26 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

“Mechi dhidi ya Asas bado haijaisha kama ambavyo watu wengi wanadhani, michezo hii ya Kimataifa inahitaji umakini sana ili uweze kwenda kwenye hatua inayofata na sisi hatuwezi kumdharau mpinzani yoyote yule hata kama tumefunga mchezo wa awali,”amesema Kamwe

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Agosti 20 Yanga ilishinda mabao 2-0.

Kamwe amesema malengo ya Yanga msimu huu kimataifa ni kuhakikisha inatinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika, mashindano ambayo haijashiriki kwa muda mrefu.

Related Articles

Back to top button