Wasusi wajitambulisha BASATA

Chama cha Wasusi Tanzania chaja na Mkakati wa kukuza sekta ya ususi.
DAR ES SALAAM: Katika hatua muhimu kwa sekta ya ususi nchini, Chama cha Wasusi Tanzania kimejitokeza rasmi kutambulisha chama chao kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya wasusi na taasisi za serikali ili kuleta mageuzi katika sekta ya ulimbwende na utanashati.
Akizungumza na katika kikao hicho Katibu Mtendaji wa BASATA, Dk Kedmon Mapana, amewapongeza wanachama chama hicho kwa hatua hiyo muhimu.
“BASATA inatambua mchango wa sekta ya ususi katika maendeleo ya sanaa na ajira na hivyo imefanya maboresho kwenye kanuni zitakazowatambua rasmi wasusi kama sehemu ya sekta ya urembo na mitindo nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa BASATA, Bwana Edward Buganga, ambaye pia amewapongeza kwa uamuzi wao wa kuunda chama chenye maono.
Alibainisha kuwa “BASATA iko tayari kushirikiana nao na kuwapa usaidizi kuhakikisha sekta ya ususi inakua na kutambulika rasmi.
Aidha Viongozi wa Chama cha Wasusi walijadili masuala muhimu na kusema kuwa wana ajenda zao wanazozitazamia.
Wamesema kuimarisha umoja wa wasusi nchini Chama kinapanga kushirikiana kwa karibu ili kuboresha mazingira ya kazi na kuinua sekta kwa ujumla.
Wameomba kupata fursa za kiserikali chama kinapendekeza wasusi waweze kufikiwa na miradi ya serikali inayolenga kusaidia sekta ya ujasiriamali na sanaa.
Mpango wa upangaji wa bei Ili kuhakikisha viwango vya huduma vinakuwa thabiti na wasusi wote wanapata malipo stahiki kwa kazi zao.
Katika hotuba yao, viongozi wa chama wamesema kuwa sekta ya ususi ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na wanawake, hivyo wanaomba serikali kuongeza nguvu katika kuiendeleza. Pia, waliwahimiza wamiliki wa saluni kote nchini kujisajili rasmi ili kupata fursa mbalimbali kama zilivyo sekta nyingine za kazi.




