Mitindo

Mobetto afunguka siri ya kupata michongo

DAR ES SALAAM: Mwanamitindo Hamisa Mobetto amesema mtindo wake wa maisha ndio siri ya kupata fursa mbalimbali kwenye maisha huku akitamba kuwa ndicho kinachomtofautisha na wasanii wengine.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati akitambulishwa kuwa balozi wa Azania kupitia bidhaa ya Spaghetti amesema juhudi zake katika kazi zimemwezesha kupata fursa mbalimbali.

Hamisa amesema huenda kwa kuwa yeye anapenda kula imekuwa rahisi kwake kupata fursa kama hiyo.

Amesema licha ya kwamba yeye ni mwanamitindo hapendi kujibana kula kama wengine anahitaji kujenga afya yake ili kuwa katika muonekano mzuri zaidi.

“Kila mtu anavitu anavipenda, napenda kula na ndio maana nafanya kazi kwa bidii na Mungu ananipa fursa kama hizi za ubalozi wa bidhaa za tambi, niwashukuru Azania kwa kunikaribisha kuwa mwanafamilia niwaahidi sitawaangusha nitafanya kazi vizuri,”amesema.

Amesema kampuni hiyo imekuwa ikitoa mchango kupitia kulipa kodi, kutoa ajira na kuwezesha biashara mbalimbali kupitia mauzo huku  wakitangaza fursa kwa wale wanaotaka kufanya nao kazi kuwatafuta.

 

Related Articles

Back to top button