Filamu

Waigizaji kutamba kwenye tuzo za tamthilia

DAR ES SAALAM: Bodi ya Filamu Tanzania imeshiriki katika utambulisho wa ujio wa Tuzo za Tamthilia Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuunga mkono jitihada za wadau wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini  na kukuza Sekta ya Filamu.

Utambulisho huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Tuzo hizo Elia Mjatta amesema lengo la kuanzisha Tuzo hizo ni kutambua mchango wa waandaaji wa Tamthilia na kuhamasisha uandaaji wa kazi bora na zenye ushindani ndani na nje ya nchi ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kutangaza vivutio vyetu pamoja na lugha ya Kiswahili.

Tuzo hizo zitazinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti, 2024 katika hoteli ya Serena, ambapo kilele chake kitakuwa ni tarehe 31 Oktoba, 2024. Aidha, Kwa kuanzia Tuzo hizo zitahusisha tamthilia za ndani na zinazotoka nje ya nchi ambazo zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili zinazooneshwa kwenye Televisheni za Tanzania pekee.

Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Uhakiki kutoka Bodi ya Filamu Bi Boppe Kyungu amesema Serikali kupitia Bodi hiyo inazitambua Tuzo hizo, ambapo pamoja na mambo mengine, amewataka wadau wa Filamu nchini kuungana katika kuzifanikisha  kwani tuzo ni nyenzo ya kuboresha Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button