La Liga

Vini Jr alimwa adhabu

MADRID: MCHEZAJI wa Real Madrid, Vinicius Junior, amepewa adhabu ya kutocheza mechi mbili baada ya kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa La Liga dhidi ya Valencia.

Tukio hilo lilitokea dakika ya 77, ambapo Vini Jr aligombana na kipa Dimitrievski baada ya kudaiwa kujirusha ili apate penati. Kipa huyo alimshika Vini mgongoni na kichwani, na Vini akajibu kwa kumsukuma usoni, jambo lililosababisha kupewa kadi nyekundu.

Adhabu hiyo inamaanisha Vini Jr atakosa mechi dhidi ya Las Palmas na Valladolid lakini ataruhusiwa kucheza kwenye mchezo wa Supercopa de España dhidi ya Mallorca Alhamisi ijayo. Awali, kulikuwa na hofu kuwa angeweza kufungiwa hadi mechi 12, lakini adhabu imepunguzwa hadi mechi mbili pekee.

Vini Jr amekuwa akikumbana na changamoto kubwa dhidi ya Valencia, ikiwa ni pamoja na matusi ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo. Tukio kama hili lilitokea pia Mei 2023 kwenye uwanja huo wa Mestalla, ambapo mchezo ulilazimika kusimama kwa muda kutokana na vitendo hivyo.

Related Articles

Back to top button