
KIGOMA:MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Almas Kasongo amesema watakuwa na ajenda zisizopungua 11 za mkutano mkuu wa kesho utatoa maazimio na maelekezo ya mwaka ujao.
Kasongo amesema katika mkutano huo utashirikisha viongozi wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Championship na Ligi Daraja la kwanza (First Division League) zamani ligi daraja la pili.
Amesema moja ya ajenda ya mkutano huo ni kutoa maazimio na maelekezo ya mwaka ujao, kutokuwa na uwasilishwaji wa bajeti na matumizi ya fedha za mwaka ujao.
“Kutakuwa na taarifa zilizokaguliwa na mkaguzi wa nje pamoja na hatuba ya Mwenyekiti wa bodi kutoa muelekeo wa mwaka ujao,” amesema Kasongo