‘Tanzania itaweka Historia CHAN’

DAR ES SALAAM: KATIBU wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wilfred Kidau amesema kusogezwa mbele kwa michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kunatoa muda wa timu ya Taifa Stars kufanya maandalizi ya kutosha.
Michuano ya CHAN ilisogezwa mbele baadala ya Februari 1 hadi 28 sasa yatafanyika Agosti, 2025, Tanzania, Kenya na Uganda ni nchi wenyeji wa mashindano hayo.
Amesema wachezaji watapata nafasi nzuri zaidi kupitia michezo mbalimbali ya kimataifa kwa ngazi tofauti kuendelea kuwajengea wachezaji uzoefu mkubwa kabla ya michuano ya CHAN mwezi Agosti.
“Kwa mujibu wa kalenda ya michezo mikubwa ya timu ya Taifa Stars tutakuwa na mechi mbili za kutafuta kufuzu fainali za kombe la Dunia tutacheza Machi, mwaka huu.
“Kwa sababu tunapata maandalizi ya kutoka ninaimani nchi yetu itaweka historia kwenye CHAN, tutacheza fainali na ikiwezekana kutwaa ubingwa,” amesema.