CAF yaongeza za zawadi za CHAN

DAR ES SALAAM: SHIRIKISHO la mpira wa miguu Afrika (CAF) imeongeza fedha za Tuzo kwa asilimia 75 kwa mshindi wa michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN), yatakayofanyika Tanzania, Kenya na Uganda 2024
CAF imetangaza kuwa pesa ya mshindi wa jumla ya michuano ya CHAN imeongezeka kwa asilimia 75 na mshindi sasa anapata dola million 3.5 na zimeongezwa hadi dola milioni 10.4 ikiwa ni ongezeko la 32%.
Rais wa CAF, Patrice Motsepe amesema: “Tunafuraha kuhusu michuano ijayo ya CHAN itakayofanyika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda na tumeongeza kwa kiasi kikubwa pesa za mshindi hadi dola milioni 3.5 ambalo ni ongezeko ya 75%.
Pia tumeongeza jumla ya pesa hadi dola milioni 10.4 ambalo ni ongezeko la asilimia 32, CHAN ni Mashindano muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa wachezaji wa soka barani Afrika na wachezaji chipukizi wenye vipaji na yatachangia pakubwa katika ushindani wa kimataifa wa soka la Afrika na Mashindano ya CAF.
Amesema mashindano haya ni sehemu ya mkakati wa CAF wa kuwekeza katika soka la Afrika na kuifanya kuvutia na kuvutia mashabiki wa soka, wadhamini, washirika na wadau wengine barani Afrika na duniani kote.
Michuano ya CHAN itaanza Jumamosi Februari Mosi hadi 28, 2025 ambayo ni fainali, nchini 17 tayari zimefuzu kucheza fainalia hizo ni Kenya Tanzania, Uganda, Morocco, Guinea, Senegal, Mauritania, Niger, Burkina Faso, Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kongo, Sudan.Zambia, Angola na Madagascar.