Takwimu za Yanga, USM Alger CAF

Kuelelea mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Yanga dhidi ya USM Alger Mei 28, hizi ni takwimu za timu hizo kuanzia hatua ya makundi.
Timu hizo zimecheza michezo Kumi (10) hadi sasa.
Yanga imeshinda michezo saba, imepoteza mmoja na kutoa sare michezo miwili, huku USM Algers ikishinda michezo mitano, sare mitatu na kupoteza michezo miwili.
Yanga imefunga jumla ya magoli 15 hadi sasa kwenye michuano hiyo.
Imefunga mabao tisa katika uwanja wa nyumbani huku ikifunga sita viwanja vya ugenini.
Yanga imeruhusu jumla ya mabao Matano.
Mabao manne imeruhusu katika viwanja vya ugenini, huku ikifungwa bao moja kwenye uwanja wa nyumbani.
USM Alger imefunga jumla ya mabao 17
Mabao 13 imefunga katika uwanja wa nyumbani huku ikifunga mabao manne kwenye viwanja vya ugenini.
USM Alger imeruhusu nyavu zao kuguswa mara nane, mabao saba imefungwa katika viwanja vya ugenini huku ikiruhusu bao moja tuu kwenye uwanja wa nyumbani.
Mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la shirikisho Afrika baina ya timu hizo mbili utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam na kisha mchezo wa mkondo wa pili kupigwa Algeria Juni 3.