BurudaniMuziki

Baby J kurudi upya kwenye Bongo Fleva

BAADA ya kimya kirefu malkia wa muziki wa bongo fleva mwenye maskani yake Zanzibar, Jamila Abdullah maarufu Baby J ameibuka na kudai kuwa ameamua kurudi kwenye muziki ili kuongeza hamasa kwa watoto wa kike kuonyesha vipaji vyao vya uimbaji kupitia yeye.

”Nimekuwa nje ya muziki kwa muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali binafsi lakini siku si nyingi nitaachia wimbo wangu mpya utakao nitambulisha upya kisha nitajipanga kuachia albamu, hii itawasaidia wasichana wenye vipaji lakini wanashindwa kuvionyesha sababu hawana wa kuonysha kama mfano katika muziki,” anasema Baby J.

Akizungumzia ujiowake mpya Baby J anasema utakuwa na utofauti kulingana na soko la muziki huo kwa sasa linavyotaka.

nitaanza na wimbo wa kunitambulisha upya na haitochukua muda mrefu nitaachia albamu yangu itakayokuwa na mshindo mkubwa itakuwa suprise, waandishi wa media zote nitawaalika, muziki hauachiki sasa nipo tayari kurudi katika nafasi yangu ya umalkia wa muziki wa bongo fleva kwa Zanzibar na bara maana huku Zanzibar muziki haupigi hatua kubwa hasa kwa watoto wa kike” anasema Baby J.

Baby J amewahi kutoa nyimbo mbalimbali akiwa amewasikilizisha wasanii wenye majina makubwa katika muziki wa bongo fleva na nyimbo hizo zikafanya vizuri ukiwemo wimbo wa ‘Moyo wangu umechoka’ aliomshirikisha Pasha, ‘Nitembee’ aliomshirikisha Chid Benz, ‘Bwashehe aliomshirikisha Ally Kiba, ‘Mpenzi wangu’ aliomshirikisha Banana Zoro pamoja na ‘Bomoa bomoa’ aliomshirikisha Bob Junior.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button