BurudaniMuziki

Kala: Vijana wekezeni kwenye vipaji, ubunifu

RAPA Kala Jeremiah amesema licha ya hamasa ya kuwataka vijana wasome kwa bidii ili kuwa na maisha mazuri ya baadae lakini pia wazazi wanatakiwa kuwapa muda vijana ili wawekeze katika ubunifu na vipaji walivyonavyo kwa sababu teknolojia inavyozidi kukua soko la ajira linapungua.
Kala anasema Serikali inatakiwa iweke mazingira ya namna vijana wataweza kuendeleza vipaji vyao na ubunifu walionao bila kuwa na vikwazo visivyo vya lazima kwa sababu teknolojia ndipo inapotupeleka katika kutegemea vipaji na ubunifu kwa vijana.
“Vijana wasome sana wanavyosoma vitakuja kuwasaidia katika maisha yao lakini pia wasisahau kuwekeza katika vipaji vyao huku wakiweka mbele bunifu zao maana vitu vikubwa duniani vyenye fedha nyingi ni vya wabunifu na wenye vipaji na si wenye ajira, ndiyo maana wanamichezo wengi wanaongoza kwa kipato kikubwa sababu ya vipaji na matajiri wengi wakubwa wanaongoza kwa sababu ya bunifu zao” amesema Kala Jeremia.
Kala aliyewahi kujizolea tuzo tatu kupitia wimbo wake wa ‘Dear God’ ameongeza kwa kuwataka wazazi kutowazuia watoto wao wanapotaka kuonyesha vipaji vyao kwa jamii kwa sababu vipaji na ubunifu ndiyo mtaji mkubwa wa maisha ya baadae ya kijana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button