Soka la ufukweni waliwaka 2024

MWAKA 2024 umekuwa wa kihistoria kwa maendeleo ya soka Tanzania ukionesha ukuaji mkubwa wa michezo kupitia mafanikio ya klabu na timu za Taifa.
Tanzania inajivunia kuwepo kwa Timu ya Taifa ya soka la Ufukweni ambayo imekuwa sehemu ya hadithi ya kupendeza kwa Taifa kuwa miongoni mwa timu zilizofuzu fainali ya Mataifa ya Afrika BSAFCON 2024, yaliyofanyika nchini Misri.
Timu ya soka la Ufukweni ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo mikubwa imekuwa mwakilishi pekee kutoka ukanda wa CECAFA ilipangwa Kundi A na Morocco, Misri na Ghana.
Tanzania haikuambulia ushindi katika michuano hiyo kwa kupoteza mechi zote na kuondolewa mapema katika hatua ya makundi.
Ikumbukwe kwamba mashindano ya BSAFCON, sehemu ambayo mataifa shiriki hutafuta nafasi ya kucheza fainali za kombe la Dunia mwaka 2025.
Mashindano hayo ya kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza, kisiwa cha Shelisheli kitakuwa mwenyeji.
Kushindwa kufanya vizuri katika michuano hiyo ya BSAFCON, Tanzania imepoteza sifa ya kwenda kushiriki michuano hiyo ya kombe la Dunia mwakani.
Fursa kwa wachezaji kujiuza:
Licha ya kushindwa kucheza fainali lakini BSAFCON imekuwa sehemu ya baadhi ya wachezaji kujiuza kwa kusajiliwa na klabu nje ya Tanzania.
Aliyekuwa kocha na pia mchezaji, Jaruph Juma ni miongoni wa wachezaji walipata nafasi ya kusajiliwa na klabu ya Ain Diab, Casablanca inayoshiriki Ligi ya mchezo huo nchini Morocco.
Jaruph ameeleza kuwa ni mara ya kwanza kwaTanzania kucheza kushiriki michuano hiyo lakini licha ya kuondolewa mapema imewasaidia wachezaji kupata uzoefu na kufanikiwa kusajiliwa.