Kwingineko

Italia yawasilisha orodha ya viwanja 14 vitavyochezewa Euro 2032

ROMA: SHIRIKISHO la soka la Italia (FIGC) limewasilisha kwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) orodha ya viwanja 14 vinavyopendekezwa kuandaa mechi za Mashindano ya Euro 2032, ambayo yatafanyika kwa pamoja nchini Italia na Uturuki.

Hatua hiyo inaweka rasmi viwanja hivyo katika mchakato wa kuwania nafasi ya kutumika katika mashindano hayo makubwa ya soka barani Ulaya.

Kwa mujibu wa mpango huo, UEFA sasa itapitia na kutathmini viwanja vilivyowasilishwa kabla ya FIGC kufanya uteuzi wa mwisho wa viwanja vitano vitakavyotumika nchini Italia wakati wa Euro 2032.

Viwanja hivyo 14 vimetawanyika katika miji 13 ya Italia, hatua inayolenga kuhakikisha mechi za mashindano hayo zinafanyika katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Miji iliyowasilisha viwanja katika mchakato huo ni Bari, Bologna, Cagliari, Florence, Genoa, Lecce, Milan, Naples, Palermo, Roma, Salerno, Turin na Verona.

Miji yenye historia kubwa katika soka la italia iliyowasilisha viwanja vyake ni Roma, Milan, Naples na Turin. Hata hivyo, viwanja vyote 14 vitapitia mchakato wa tathmini kabla ya uamuzi wa mwisho kufanyika.

Baada ya UEFA kukamilisha tathmini yake, FIGC itachagua viwanja vitano vya Italia vitakavyotumika katika Euro 2032, huku mashindano hayo yakiandaliwa kwa pamoja na Italia na Uturuki.

Related Articles

Back to top button