Simba wasema hawajamaliza, kushusha ‘Mashine’ nyingine

DAR ES SALAAM: LICHA ya kutambulisha nyota 10 wapya, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori ameweka wazi kubwa bado wanaendelea kushusha vifaa vingine vipya kwa ajili ya kutengeneza timu imara.
Amesema usajili haujakalimika na wanaendelea kuongeza watu kulingana na mahitaji ya timu yao na huku kuendelea kupunguza wachezaji kupisha maingizo mapya.
Baadhi ya wachezaji ambao Simba imewasajili ni pamoja na Lameck Lawi, Abdulrazack Hamza, Debora Fernandes, Augustine Okejepha, Ahoua Jean Charles, Steven Mukwala, Joshua Mutale na Valentino Mashaka.
Kwa mujibu wa Mjumbe huyo Simba inahitaji kutengeneza timu mpya na kusajili wachezaji kulingana na vigezo ikiwemo umri wa wachezaji ambao watakuwa katika mipango yao ya muda mrefu.
“Tulihitaji kuwa na timu mpya, tukafanya mabadiliko makubwa, ukichelewa kubadilisha timu muda mrefu lazima yatokee haya yaliyotkea msimu uliopita
Tunaangalia mchezaji sio kwa mechi moja tulitulia na kujiridhisha juu ya usajili wetu, kuna mambo makubwa yanakuja, Tumetumia wataalamu kufanya mabadiliko ya timu tunaamini vijana wenye vipaji na muda mfupi wanaweza kupeperusha bendera ya Taifa,” amesema Magori.
Kuhusu vijana wanaosajiliwa kushindwa katika mfumo, amesema Simba na Yanga zinapresha kubwa, usipopata kocha hodari ya kuwapa nafasi wachezaji wageni na vijana katika kikosi cha kwanza, yanatokea kila baada ya miezi sita unamtoa kwa mkopo.
“Misimu mitatu Simba haijakosea kwenye usajili bali hatukuweza kushinda, kuna mambo matatu yanayotokea kushindwa kufanya vizuri kwanza kupata mwalimu mzuri anayethubutu kufanya mzunguko wa wachezaji , wachezaji wazuri na uongozi madhubuti,” amesema Magori.
Kuhusu ishu ya Lawi, Magori amesema “Lameck Lawi imekuwa tatizo tumelipa timu na mchezaji lakini lipo kwenye mamlaka husika tuwaachie wao ndionwatakao amua, msimamo wetu kuwa tumemsajili mchezaji kutokana na mahitaji ya timu,”
Magori pia amekanusha taarifa za kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo kurejea akisema hakuna ukweli wowote juu ya Pape Sakho kurejea kwa sababu hakuwahi kumjadili na ni ngumu sana kuzungumzia, kuhusu Aishi Manula mjumbe huyo amesema suala lake lipo kwenye ofisi ya Mtendaji Mkuu, Mosses Phiri alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na baada ya miezi sita tumekubaliana kumalizana kisalama na hakuna kesi itakayoenda fifa,” amesema Mjumbe huyo.
Ameeleza kuwa Aubin Kramo wapo kwenye mazungumzo na kuweza kuachana na kumpeleka kwa mkopo baada ya kuona msimu uliopita hakucheza msimu mzima na kuhofia kumpa presha ya mashabiki.