Ligi Kuu

Filamu ya Chama mwaka 2024

DAR ES SALAAM: USAJILI wa kiungo wa Yanga Clatous Chama kwenda kutoka Simba ulitikisa nchi kwa mwaka 2024 huku mashabiki wa pande zote mbili wakiwa roho juu.

Kiungo huyo wa Kimataifa wa Zambia, aliachana na Simba baada ya mkataba wake kufikia tamati.

Licha ya wachezaji wengi kuhusishwa na baadhi ya timu lakini, sakata la kiungo huyo kwenda Yanga liliingia kwenye sura mpya mashabiki wa klabu hizo mbili kongwe waliingia katika sintofahamua juu ya kiungo huyo.

Chama anayezungumziwa hapa yule aliyejenga jeshi kubwa ndani ya Simba, amekuwa kipenzi cha mashabiki na wadau wakubwa wa klabu hiyo tangu alipojiunga mwaka 2017 akitokea Zesco United, Zambia.

Nyota ambaye amefanya makubwa ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi katika michezo ya ndani na kimataifa ambayo Simba imekuwa ikicheza, hakuna mtu anayebisha juu ya msaada wa kiungo huyo na klabu hiyo.

MKATABA WA CHAMA NA SIMBA:

Chama amejiunga na Yanga akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake wa miaka miwili na Simba kufikia tamati, Juni 30, 2024 klabu hiyo ikaamua kutomuongezea mkataba.

Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja tetesi za Chama kuhusishwa kujiunga na Yanga zilikuwa zikisambaa kwa kasi ikitajwa kwamba Simba haikuwa na mpango wa kumpa mkataba mpya.

Tetesi ambazo zilifanya mashabiki wa timu hizo mbili kutoelewa kuwa kiungo huyo kuhusishwa kwa muda mrefu kusajili na Yanga lakini ziligonga mwamba hatimaye 2024 kufanikiwa kuinasa saini yake.

SAKATA LA CHAMA ILIPOANZIA:

Meneja wa Idara ya Habari wa Simba. Ahmed Ally alibainisha kuwa mchezaji huyo bado hajasaini kusalia ndani ya klabu hiyo huku mazungumzo ya awali ya kusaini mkataba mpya yakigonga mwamba.

Utata ulianza kuibuka baada ya mabosi wa Simba kugawanyika baadhi ya viongozi wa timu hiyo waliona inatosha na hawapaswi kuendelea naye kwa kuwa wanataka kujenga timu mpya.

Misimu mitatu mfululizo, viongozi na mashabiki wengi walikuwa wanamtazama Chama kama mtu ambaye amepoteza mapenzi na Simba na kuwatumikia kwa sababu ya fedha.

Licha kuwepo kwa mvutano huo wa ilidaiwa mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji alitoa nafasi wa wajumbe wake anayemtaka kiungo huyo yupo tayari kumuongeza mkataba.

MAAMUZI MAGUMU:

Baada ya kusikia tetesi za kwamba Mo Dewji ametoa nafasi ya kiungo huyo kujadiliwa na kutaka kupindua meza kuliwepo kwa mgawanyiko wa viongozi juu ya nyota huyo maamuzi magumu yalipita.

Uamuzi wa kumuacha Chama ulikuwa mgumu kwa viongozi kwa vile walikuwa wanaogopa presha na lawama kutoka kwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo kutokana na mahaba makubwa ambayo walikuwa nayo kwa nyota huyo kutoka Zambia.

YANGA KUMTAMBULISHA:

Ilikuwa Julai Mosi, 2024, Yanga walikata mzizi wa fitna na kushusha presha ya mashabiki wao kwa kumtambulisha rasmi kiungo huyo baada ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

Ilikuwa furaha kwa mashabiki wa Yanga juu ya ujio wa nyota huyo, utambulisho wake ukiwa mara mbili. Moja akiwa nchini kwao Zambia ambao ilikuwa Julai Mosi, ambao akiwa na nguo za nyumbani na baadae walimtambulisha na jezi ya Yanga jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button